By Nelly W Waweru
Mwanangu nasema nawe,
Wosia huu kaupokee,
Keshoye tauhitaji,
Utumie kwa makini,
Mama alisema, leo hii natafakari.

Maadili mema zingatia,
Siwe mwana jeuri,
Sheria ino makali,
Takutia pinguni,
Mama alisema, akilini meyaweka

Maisha haya ni zawadi,
Tulopewa na ALLAH
Simtupe Mungu wako,
Mungu si utumwa,
kumcha Mama alisema, wosia
huu nimekiri

Jifunze kutembea mwana,
Uwe huru sitegemee,
Dunia mtu mkavu,
Kiegemea taanguka,
Mama alisema, usemi wake
nauona

Asante mama kwa wosia,
Natekeleza livyosema,
Japo Mungu kakutwaa,
Mafunzo yako meniachia
Mama alisema, dunia yeye
kaondolewa

Kati tamati metimia,
Kalamu naweka chini,
Kumbukumbu za mamangu,
Naweka wazi kwa umma
Mama alisema, leo hii metimiza

Shairi: Mama Alisema