Shairi: Nidhamu

Nawapa hilo fasiri ya hili neno nidhamu,

Mukae mukikariri,muwe mkilifahamu

Kuwa ni kitu cha heri,na ambacho ki timamu

Mja asiye nidhamu,huwa anayo kasiri.

 

Ni ngao ya ujasiri,ikulindapo na mamu,

Jambo zito hilo shari, ukaliona si ngumu

Kwa kuwatia shauri, wenzio kila hirimu,

Mja asiye nidhamu, huwa anayo kasiri

 

Kuogopa morimori, wadogo hata makamu,

Na kuwa nayonadhari, uwe ukiwa heshimu,

Ndilo jambo msumari, linaloitwa nidhamu,

Mja asiye nidhamu, huwa anayo kasiri

 

Utovu wenye hatari, ambao una majukumu,

Hasa kutowapa ali, wazazi waliohudumu

Wa kuzaa kwa fahari, wakakupa na elimu,

Mja asiye nidhamu, huwa anayo kasiri.

 

Nawapa mambo dhahiri, mjue wataalamu,

Heshima chama Hariri, kinachowatawala humu,

Na serikali hadhari, sikosee hirimu,

Mja asiye nidhamu, huwa anayo kasiri.

 

Kuogopa takari, hiyo kuitoa nidhamu,

Aloziumba sayari, akakumba binadamu,

Hadi leo ushauri, ogopa sana karimu,

Mja asiye nidhamu, huwa anayo kasiri.

 

Iogope duari , sujua tabasamu,

Ndio utu mashauri , na sio wenda wazimu,

Si kuzipanga jeuri, upitapo wadhulumu,

Mja asiye nidhamu, huwa anayo kasiri.

 

Na nono jingie zuri, badili yake nidhamu,

Ni ambalo laajiri, ni adabu waaduwamu,

Na kuwa na desturi, za kupendeza kaumu,

Mja asiye nidhamu , huwa anayo kasiri

 

Nalikomeza shairi, liloeleza nidhamu,

Mukae mukitafakari , kuwa ni jamo lazimu,

Ni heshima kusubiri, ninapofunga nudhumu,

Mja asiye nidhamu, huwa anayo kasiri.

Na Sir Joe [Joe Muricho]