Poem: Forest

Najibwaga ulingoni, mwa busara kuchangia,

Mimi ndiye wa zamani, mengi nimeshuhudia,

Sasa niko uzeeni, nashangazwa na dunia,

Penye nia ipo njia, sikate tama.

 

Na iwapo ni shuleni, masomo yanitatiza,

Usaisi masomoni, kitabu nikakimbia

Haba na haba, bongoni, elimu itaniingia,

Penye nia ipo njia, sikate tama.

 

Hapo mawimbini, nawe hapo pigania,

Hapo ndipo upenyuni, japo mawe ya kuzuia,

Mtimia utilie kani, bandarini taingia,

Penye nia ipo njia sikate tamaa.

 

Kama kwenda uchumini,biashara wania,

Usichofu asilani, hasara ikatukia,

Leo ukazoa duni, na kesho litazidia,

Penye nia ipo njia, sikate tama.

 

Beti ya tano naifikieni, nyongeza kuwachia,

Rabuka wajalieni, rehema awazidia,

Taifa lawahitajini, wenu wito wachangia,

Penye nia ipo njia, sikate tama.

 

Joel Muricho (Sir Joe)