Na Ammar Kassim

Chuo Kikuu cha Kibabii kilianza kampeni yake ya kufuzu kwa michuano ya vyuo vikuu nchini (KUSA) kwa kutoka sare ya goli moja kwa moja dhidi ya chuo cha Kaimosi.
 
Kibabii ilionekana kudhibiti mchezo katika dakika za mwanzo kwa kuwapiga wenyeji Kaimosi bao la mapema. Bao hilo lilifungwa na difenda Aguastine Shikuku aliyepiga mkwaju wa ikabu uliomzidi nguvu mlinda lango wa timu ya Kaimosi.
 
Kipindi cha pili Kibabii walionekana kudhibiti mchezo hata zaidi huku bao la mshambulizi wa timu hiyo Emmanuel Munyasia Kanga kukataliwa na mshika kibendera kwa madai ya kumchezea visivyo mlinda lango wa Kaimosi.
 
Matumaini ya Kibabii yalikatizwa dakika mbili kabla ya mchuano kutamatika kwa bao la kichwa lilofungwa na mshambulizi wa Kaimosi lililotosha kuwapa Vijana wa Kaimosi sare ya 1-1
 
Saa moja baada ya mechi hio kukamilika, Kibabii ilirudi ugani kutafuta ushindi wa kwanza dhidi ya mahasimu wao wa jadi MMUST ili kujihakikishie nafasi ya kufuzu katika awamu ya pili ya mashindano hayo. Japo MMUST walionekana kudhibiti sehemu kubwa ya mchezo huo, Vijana wa Davis Jumbo walijizatiti na kuandikisha sare tasa 1-1 katika kipindi cha kwanza.
 
Mambo yalibadilika Kipindi cha pili, wakati difenda wa timu ya Kibabii Augustin Shikuku alipojifunga goli lililotosha kuwapa MMUST ushindi muhimu wa 1-0.
 
Nafasi ya chuo Kikuu cha Kibabii ya kufuzu yalibaki kwenye mechi kati ya MMUST na Kaimosi. Huku ushindi wa magoli 2-1 wa timu ya MMUST dhidi ya Kaimosi ukipenyeza timu zote mbili kwenye awamu ya pili ya kipute hicho kwa sheria ya magoli ya kufungana.
 
Awamu ya pili ya dimba hilo itaendelea mwanzoni mwa mwaka ujao katika uga utakaotangazwa baadaye.

Sheria ya Magoli ya Kufungana Yakifungia Nje Kikosi cha Kibabii katika Michuano ya KUSA

Sheria ya Magoli ya Kufungana Yakifungia Nje Kikosi cha Kibabii katika Michuano ya KUSA

Sheria ya Magoli ya Kufungana Yakifungia Nje Kikosi cha Kibabii katika Michuano ya KUSA