1.MKARIMU.

Si kawaida kwa watu wengi hasa wale waliopata umaarufu kutangamana na watu wasowajua.Lakini hilo ni tofauti kabisa na Zainab Ismail.Kwenye safari yake ya siku tatu chuoni Kibabii,hakuwa karibu na wanafunzi pekee bali pia wafanyakazi wa chuo wakiwemo wapishi na walinzi.
 

2.MCHESHI.

Si bure aliajiriwa NTV. Zainab Ismail ni ‘Churchill’ tosha.
Usiwe karibu naye kama huezi vumilia maumivu ya mbavu.Utacheka hadi ukome!
 

3.MUWAZI.

Zainab hafichi ukweli kwa atakae taka kuujua.Muulize kuhusu safari yake ya uanahabari na atakueleza bila kukuficha.Ila si kwa yeyote tu,kwa yule ambaye ameonyesha hamu na hamumu.
 

4.MREMBO.

Hapa nilisita kuandika kiasi,lakini ilinibidi nipige moyo konde.Zainab anavutia si haba.
Sawa,vipodozi huongeza urembo lakini huu wa Zainab ni tofauti.Kilicho na sifa kipewe sifa.
 

5.HUTHAMINI MASHABIKI WAKE.

Mwitishe selfii na jibu litakalomtoka mdomoni ni moja tu; ‘sure’.
Wakati mwengine hata huwapunguzia kero wale waoga wa kuomba selfii.
Watu wanapomzingira,swali lake huwa moja “Do you want a selfie?”.
 

6.NI MLUMBI HODARI.

“Nekesa” (Jina alilobatizwa kwenye safari yake katika kaunti ya Bungoma) ni mlumbi hodari Sana.Anapokuhadithia hadithi au visa kuwahusu watu,utatamani kusikia tena na tena.

Mtindo wake wa kueleza visa hivi ni wa aina yake.Ila wajua sababu? Zainab binafsi ni mpenzi wa visa kuwahusu watu. (Human interest stories)
 
7.NI MCHAPAKAZI.

Wengi walianza ¬†kumfahamu Zainab pindi alipojiunga na NTV na kujumuishwa Travor ¬†Ambija kwenye matangazo ya “Weekend Edition”.Si siri alikuwa gumzo na kila mtu akawa anamsifia kwa umahiri wake wa lugha ya kimombo.

Lakini hakuanzia hapo,kwa wale ambao walikuwa wanafwatilia “The presenter season 2” kwenye runinga ya KTN mwaka wa 2015,watakubaliana nami kuwa kujituma kwake ndo ilikuwa sababu ya yeye kuibuka kwenye idadi ya watangazaji kumi walichaguliwa na kati ya elfu sita waliojitokeza kutafuta nafasi za ajira.

Ukidhani kuwa uchapakazi wake ni kazini ama wakati wa kutafuta ajira pekee,umejidanganya. Kutana nae ana kwa ana utafahamu ninayokwambia.Sisemi sana nikaharibu!

 

Hizo ni baadhi ya vitu tulivyovigundua ndani ya siku tatu pekee.Ila Zainab Ismail ni zaidi ya hayo.
Na AMMAR KASSIM

Vitu Saba Tulivyogundua Kumhusu Zainab Ismail wakati wa